Polepole: Tunafanya mabadiliko ndani ya CCM makusudi

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema chama hicho kimeanza kufanya mageuzi ya makusudi ili kurejea kwenye misingi ya kuanzishwa kwake.


Katibu huyo mpya wa itikadi na uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM, amesema mageuzi hayo yanakusudia kukifanya kuwa cha watu, kuwasikiliza na kusimamia masilahi ya wanyonge ili kurejesha imani kwao katika vitendo vyote vya chama.

Polepole alisema hayo jana katika mahojiano na kituo cha redio cha Uhuru FM kinachomilikiwa na chama hicho tawala.

Chapisha Maoni

0 Maoni