Diamond: Nimesikitishwa sana kuto-shoot wimbo na Jay Z

Jana pande za Mlimani City kilinuka mbaya baada ya team nzima wa WCB Wasafi kuwepo pande hizo ikiwa ni katika suala la uuzaji wa tiketi za show ambayo ina happen leo hii pande za Jangwani Sea Breez.

Team nzima ya XXL pia ilikuwepo pande hizo ikiwa inarusha LIVE kipindi chao kutoka maeneo hayo na kupata nafasi ya kufanya interview na wasanii hao wa WCB.
Moja kati ya maswali ambayo B Dozen alimuuliza Diamond Platnumz ni pamoja na kitu gani ambacho alidhamiria kukifanya kwa mwaka huu wa 2016 ambao unaenda ukingoni lakini imeshindikana kukifanya.
“Kitu ambacho sijakifanya ni kuto kushoot wimbo wangu na Jay Z, inawezekana ikawa ni tatizo hilo pia.” Ndio yalikuwa majibu ya Diamond Platnumz akiwa anajibu swali hilo la B Dozen.
Bonyeza play kwenye video hii hapa chini ili kumsikiliza Diamond akifunguka juu ya hilo.

Chapisha Maoni

0 Maoni