LOWASA, LISU, PATROBAS KULINDIMA NDANI YA AFRICAN DREAM DODOMA JUMAMOSI HII!





Ni habari njema kwa wakazi wa Dodoma na chuo kikuu cha Dodoma kwa ujumla kuwa, siku ya tarehe 23 Aprili kutakuwa na kongamano la kukata na shoka ambapo
wanasiasa nguli kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA chini ya mwavuli unaounda vyama vinne vya upinzani al maarufu kwa jina la ukawa Mh. E. N. Lowasa, Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lisu, Mwenyekiti wa baraza la vijana CHADEMA Ndg Patrobas Katambi na wengine wanatarajiwa kuendesha kongamono la vijana litakalofanyika ndani ya ukumbi wa Africa Dream jumamosi hii ya tarehe 23 Mwezi Aprili.

Kwa mujibu wa tangazo, wanasiasa hawa watafanya kongamano kubwa la vijana ambalo litakwenda sambamba na utoaji semina elekezi na kadi za uanachama bila gharama.

Hakika hii si ya kukosa...!!

Chapisha Maoni

0 Maoni