TANZIA: PAPA WEMBA AFARIKI DUNIA, AANGUKA JUKWAANI. WAAFRIKA WENGI WAGUSWA NA KIFO CHAKE.

Mwanamziki maashuhuri wa Rhumba nchini Kongo, Papa Wemba amefariki dunia baada ya kuanguka jukwaani alipokuwa akitumbuiza mjini Abidjan, Ivory Coast. Tukio hilo lilitokea jumamosi ambapo alikuwa akitumbuiza katika kongamano la Muziki.

Waziri w
a utamaduni nchini Kongo Baudouin Banza Mukalay  amethibitisha kifo cha msaani huyo leo ambapo amesema, kifo cha msanii Wemba ni pigo kubwa nchini Kongo na Afrika kwa ujumla.

Kifo cha msanii Wemba kimepokelewa kwa masikitiko
makubwa na waafrika mashabiki wa muziki wa Rhumba ambapo kila mmoja ameeleza masikitiko hayo. 

"kitu ambacho nakikumbuka kwa Papa Wemba ni jinsi ya uimbaji wake na ukweli ni kwamba, alikuwa anauweka muziki wa kiafrika katika ramani ya dunia. Naamini alikuwa mwanamziki mkubwa". Amesema Suzana Omiyo, mwanamziki mjini Nairobi.

Mungu ilaze mahali pema roho ya marehemu.

Chapisha Maoni

0 Maoni