PICHA: ZITTO ABONGA NA WANA WA KIGOMA WALIOKO BOSTON

Chai ya asubuhi na wana  Kigoma Mjini waliopo Boston Jana. Nimefurahi sana kupata fursa ya kubadilishana Mawazo na pastor Mlongecha na ndugu zangu wengine kuhusu Jimbo letu.
Kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo na mbunge wa Kigoma mjini Mhe. Zuberi Zitto Kabwe ameweka picha katika ukurasa wake wa Instagram na Twitter akiwa kwenye chakula cha asubuhi mjini Boston na wana kadhaa wa kigoma. Kiongozi huyu ameweka picha hii jana akishukuru kwa nafasi ya pekee kuongea na wanakigoma wanaoishi Boston na kusisitiza kuwa angependa washirikiane katika kulisongesha gurudumu la maendeleo ya Kigoma na Tanzania kwa ujumla.

Chapisha Maoni

0 Maoni