PARESO: MAWAZIRI WANAFANYA KAZI KAMA VICHAA NA ZIARA ZAO ZA KUSHTUKIZA.

Wakati suala la utumbuaji majipu likipamba moto katika uongozi wa awamu ya tano, Mbunge wa viti maalum (CHADEMA), Bi. Cecilia Pareso apigilia msumari kwa mawaziri wa awamu ya tano. Bi. Pareso asema, mawaziri wanafanya kazi kama vichaa na ziara zao za kushtukiza na kusababisha nchi kuongozwa kinyume cha misingi ya uongozi wa sheria.

Kauli hizo amezisema leo kwenye ukumbi wa African Dream kwenye kongamano la vijana BAVICHA NA CHASO lililofanyika leo tarehe 23 mjini Dodoma ambapo amefafanua madhaifu kadha wa kadha wa uongozi wa awamu ya tano chini ya rais JPM ikiwa ni pamoja na kuwafukuza wafanyakazi bila utaratibu wa kisheria.

"...mahakamani wanashinda kwa sababu wanafukuzwa kinyume cha sheria..." amesema Bi. Pareso.

Katika hatua nyingine, ameilalamikia pia serikali kwa suluhu za jukwaani katika migogoro ya ardhi, kitu ambacho amesema hakiwezi kuleta suluhu ya kudumu.

"...migogoro ya ardhi, waziri anarudisha ardhi kwa mdomo ni siasa nyepesi...". Amesema.

Mhe. Cecilia pia ameilaumu serikali kujiapiza kwa kukuza uchumi wa nchi kwa 7.2% wakati wananchi wanaishi katika umasikini wa kupindukia na bei ya sukari kuendelea kupanda hali kadhalika huduma duni kwa wananchi.

Chapisha Maoni

0 Maoni