HALI YA USAFIRI CHUO KIKUU CHA DODOMA YATISHA, WANAFUNZI WAPITIA MADIRISHANI KUWAHI NAFASI.

Shida ya usafiri katika chuo kikuu Dodoma imekuwa kero ya aina yake ambayo inachukua sura mpya siku hadi siku. Hii ni kutokana na uhaba wa magari-daladala, hali ambayo imekuwa ikiwafanya kukaa muda mrefu bila kupata usafiri na hata usafiri huo ukitokea, shida imekuwa kuwahi nafasi ili kila mmoja kuhawi kwenye shughuli zake za kila siku.

Camera yetu imefanikiwa kunasa picha kadhaa ambazo baadhi
ya wanafunzi hawa wamelazimika kupitia kwenye madirisha ya gari ili kuwahi nafasi na kuwahi kwenye shughuli zao za kila siku. Kituko hiki cha aina yake kimeshuhudiwa na blogger leo tarehe 23 kwenye kituo kidogo cha daladala Block  T. COED.


TAZAMA PICHA ZAIDI ZA KERO HII




Chapisha Maoni

0 Maoni