WAITARA AIBWATUKIA SERIKALI. ADAI KAMA WALIONA TBC ITAGHARIMU KURUSHA MATANGAZO, WAACHE VYOMBO BINAFSI VYA HABARI VITANGAZE VIKAO VYA BUNGE MOJA KWA MOJA.

Mbunge wa Ukonga, Mhe. Mwita Waitara (CHADEMA) aitolea macho serikali ya awamu ya tano chini ya Dkt. J.P. Magufuli kuwa, kama iliona shirika la utangazaji la taifa (TBC) linagharimu, basi wavipe uhuru vyombo binafsi vya habari ikiwa ni pamoja na ITV na AZAM virushe matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge.

Mhe. Waitara amesema, kwa kuwa vyombo binafsi vya utangazaji habari kama ITV na AZAM havijawahi kuomba hela serikalini, basi serikali iviruhusu vyombo hivyo ili virushe matangazo moja kwa moja ili kuwaendea haki
wananchi juu ya haki yao ya msingi ya kupata tarifa.
“…wanaondoa taarifa ili wananchi wasipate maarifa kama waliyonayo…” amesema Mhe. Waitara.
Katika hatua nyingine, Mhe. Waitara amewataka vijana kushughulika na utoaji elimu katika majimbo ya CCM ili wananchi wajue nini wawakilishi wao wa CCM wanawafanyia. Kauli hii ameitoa kwenye kongamano la vijana lililofanyika leo katika ukumbi wa African Dream, mjini Dodoma leo tarehe 23 aprili.

Chapisha Maoni

0 Maoni