MKAPA KUIKALISHA KITAKO BURUNDI MJINI ARUSHA TAREHE 2-6 MWEZI UJAO.

Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamini William Mkapa anatajaliwa kuongoza mazugumzo na Burundi mjini Arusha kuanzia tarehe 2 hadi 3 ya mwezi Mei.
Mazungumzo hayo
yanatarajiwa kufanyika kwa ajili ya kurejesha amani nchini Burundi iliyotoweka kwa muda mrefu sasa baada ya Rais wa Nchi hiyo, Bwana Pierre Nkurunzinza kung'ang'ania madaraka, tukio ambalo lilisababisha majribio kadhaa ya mapinduzi likiwemo lililofanyika na Godefloid Niyombale, aliyekuwa mpiganaji wa jeshi la taifa la Burundi.

Kutokana na machafuko ya kisiasa nchini humo, watu wamepoteza maisha na wengine wengi kukosa makazi na kuwa wakimbizi katika nchi jirani pamoja na Tanzania.

Mazungumzo hayo ni fursa pekee ya kufikia mwafaka wa nini kifanyike katika kurejesha amani nchini Burundi.

Chapisha Maoni

0 Maoni