SIASA ZA TANZANIA NA HATIMA YA MAENDELEO YA NCHI

Siasa ndio uti wa mgongo wa maendeleo ya taifa lolote lile. Pamoja na kuwepo kwa mitizamo tofautitofauti na baadh ya watu kuchukia siasa, bila shaka ni kutokujua tu kwamba, binadamu asili yaki ni siasa, sawia kabisa na
madai ya mwanafalasafa wa Kigiriki Aristotle alivyowahi kusema katika moja ya kazi zake.

Siasa za Tanzania ni gumzo. Wapo wanaodai kuwa Tanzania imekomaa kisiasa kwa kulinganisha na nchi zingine za kiafrika. Lakini swali muhimu kabisa ni je, kwa ukomavu huu wa siasa kama inavyodaiwa, Taifa linanufaika vipi na namna hiyo ya siasa? Lakini pia, nini msimamo halisi wa siasa za Tanzania: je ni siasa za kijamaa au siasa za kibepari? Ni sehemu ipi sasa inabainisha kuwa siasa za Tanzania zitakuwa na muundo sawili kati ya miundo hii miwili? Je, tunatizama kutoka kwa nani?

Hakika maswali haya na mengine lukuki yamekosa majibu halisi. Wapo wanaaodai kuwa, Tanzania bado inafuata mfumo wa hayati J.K.Nyerere wa kijamaa chin ya azimio la Arusha la mwaka 1967. Lakini pia wapo wanaodai kuwa Azimio hili la Arusha lilikufa mapema kabisa kabla hata ja baba wa Taifa kufariki na hata yeye alithibitisha hilo katika moja ya hotuba yake alipokutana na waandishi wa habari akisema;

"mpaka sasa sijaona wapi kosa lilifanyika...natembea na vitabu viwili, biblia na Azimio la Arusha...Viongozi wetu walikutana Z,bar, wakakaa, wakakubaliana na waliporudi, hawakutuambia kitu. Walianza tu kufanya tofauti na Azimio la Arusha na sisi wenye akili tukajua hilo ndivyo tayari limekwisha kufa"

Maneno haya yanaonesha dhahiri kuwa, Azimio lilikufa kabla yake kufariki. Sasa je, kama lilikufa, Tanzania bado ni ya kijamaa? Kama ni ndiyo, ujamaa wa aina gani?

Itaendelea...

Chapisha Maoni

0 Maoni