KWA WAZAZI PITA HAPA UPATE MAWILI, MATATU JUU YA MALEZI

Tumekuwa na mada maalum nyingi za mambo tofauti kama urembo magari simu n.k. lakini hatujawahi kuwa na mada hii maalum ya watoto.

Kumlea mtoto tangu kutungwa kwa mimba mpaka kuzaliwa na hatimaye kulelewa mpaka kuvuka kile kipindi cha hatari si jambo dogo. 

Changamoto ni nyingi hasa na zingine hatujui jinsi ya kuzitatua lakini tukiwa na hii mada hapa jukwaani tutashirikishana na kujuzana mengi kwa haraka na uhakika zaidi.

Kuna vitu vidogo vidogo ambavyo havihitaji daktari au ufumbuzi wake ni kama huduma ya kwanza kabla hujapata usaidizi mwingine. 

Kwa mfano, ufanyeje;

-Mtoto anapolialia
-Mtoto anapopata gesi tumboni
-Mtoto anapopaliwa kila akila chochote
-Mtoto anaposhtuka shtuka usiku na kulia sana nk k

Hatari zimnyemeleazo mtoto;
-Umeme
-Maji
-Moto
-Mwanga wa Tv
-Simu, mawimbi yake
-Vyombo na vitu mbalimbali
-Madawa na vipodozi nk nk

Hii ni mada pana yenye mambo mengi mno.

Kwa mfano kitunguu saumu ni tiba kwa mtoto anayelia na kushtuka usiku, Kijiko cha asali ni tiba kwa mtoto anayekohoa mfululizo (ukiacha kifua na mafua), Vitu kama mahirizi ya kiunoni na mkononi havimsaidii mtoto, Muda mwingi kumvalisha mtoto nguo nyingi humsababishia nimonia n.k.

Mambo ni mengi...

IKIWAPENDEZA ITAKUWA NI MADA MAALUMU YA WATOTO..

Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha..!

Chapisha Maoni

0 Maoni