MSIGWA KUKERWA NA WASOMI WA TANZANIA, ATOA TAFSIRI YA NENO BUNGE.


Mbunge wa Iringa mjini (CHADEMA) Mchungaji Peter Msigwa amewapa rai wasomi wa vyuo vikuu nchini ikiwa ni pamoja na chuo
kikuu cha  Dodoma kuwa, waache kuiga wasomi ambao wamekuwa wakiitumia elimu yao pasi na kuiendeleza nchi, bali kunyume chake wamekuwa wanasiasa wasio na tija kwa taifa.
Mchungaji Msigwa ameyasema hayo katika kongamano la BAVICHA na CHASO katika ukumbi wa African Dream mjini Dodoma, kongamano ambalo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali toka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambapo mgeni rasmi aliyehudhuria kongamano hilo ni Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA.
Katika rai yake, Mchungaji Msigwa amewataka wanafunzi kuwa makini katika elimu yao na kuifanya iwe na tija kwa taifa na si ‘mediocres’.
“mimi huwa siamini katika midahalo ya wasomi wa vyuo vikuu na huwa siamini maprofesa kama kina Shivji…elimu kama ya kina polepole mimi naiita, academic prostituition”. Amesema Mchungaji Msigwa.

Katika hatua nyingine, Mch. Msigwa ametoa maana ya neno BUNGE kuwa ni mkutano wa hadhara wa wananchi. Tafsiri hii imekuja baada ya Mch. Msigwa kuitaka serikali ioneshe moja kwa moja vikao vya bunge ili wananchi waone nin kinaendelea kwa wawakilishi wao waliowatuma wkuwawakilisha.

Chapisha Maoni

0 Maoni