HECHE AKOSOA UTUMBUAJI MAJIPU WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO. ASEMA TANROADS KUNA MAJIPU LAKINI HAYATUMBULIWI

Mbunge wa Jimbo la Tarime Kijijini ambaye pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA), Mhe. John Heche aikosoa serikali ya awamu ya tano kwa kile wanachodai ni utumbuaji majipu.

Mhe. Heche ameyasema hayo katika ukumbi wa African Dream mjini Dodoma kwenye kongamano la BAVICHA na CHASO ambalo pia limehudhuriwa na Viongozi wa CHADEMA na CUF
leo tarehe 23 mwezi huu.
“Magufuli anacheza na freedom ya nchi”. Amesema Heche. Katika hatua nyingine pia, Heche ameitabiria serikali ya Magufuli kushindwa vibaya kutokana na kile alichokilejelea kilichowahi kutokea kwenye serikali ya awamu ya nne ya Dr J.M. Kikwete ambayo pia iliingia kwa mbwembwe na hatimaye taifa kugubikwa na ufisadi wa kupindukia.
Pamoja na mengine, Mhe. Heche amekizungumzia pia kile alichokidai kuwa rais hagusiki na haambiliki. “ukimgusa magufuli, you are an enemy”. Amesema Heche.
Lakini pia, Mhe Heche amezungumzia kuhusu Rais J.P.Magufuli kujitungia Bajeti na matumizi yake mwenyewe na kuacha kile kilichojadiliwa bungeni. “Rais Magufuli katunga matumizi yake na kuacha yaliyojadiliwa na bunge wakati posho za wabunge zinaliwa kila siku ni tatizo”. Amesema Mhe. Heche.

Katika hatua nyingine pia, Mhe Heche ameikosoa pia serikali kujitangaza kutaka kuanzisha viwanda wakati serikali haijui viwanda hivyo vitazalisha nini na umeme wa kuendesha viwanda hivyo bado unasuasua. “Je, kuna power ya kuviendesha viwanda hivyo, au vitaendeshwa kwa power bank”. Amesema Mhe. Heche.

Chapisha Maoni

0 Maoni