Utamu wa mechi ya Simba na JKT Ruvu huu hapa


Simba leo itashuka dimbani ikiwakaribisha JKT RUVU katika uwanja wa Uhuru jijini Dar Es Salaam, Simba Itashuka Uwanjani ikikumbuka mambo kadhaa kuhusu JKT RUVU na msimamo mzima wa Ligi Ulivyo.



Mtembeleaji wa KWATA UNIT BLOG Simba katika mechi ya mzunguko wa kwanza ilitoka sare ya bila kufungana na JKT RUVU hali ambayo inafanya mechi hii kuonekana itakuwa na upinzani mkubwa.

Kitu Kingine katika sare hiyo kikwazo kilikuwa kipa wa JKT RUVU Said Kipao aliyekuwa mchezaji kikwazo cha Ushindi wa Simba kutokana na kuokoa magoli mengi na kupelekea kipa huyo kuitwa timu ya Taifa.

Simba wanaingia uwanjani wakiwa na gap ya point 1 kutoka kwa watani wao Yanga, Kwahiyo Simba wataingia wakitaka kuongeza Gap la Points kwa Yanga na kufikia Points 4.

Wakati Simba wakifikiria kuongeza Gap kati yao na Yanga mara baada ya Yanga jana kutoa Sare JKT RUVU wao wataingia kwa mambo mawili makubwa, Kwanza ni kuhakikisha wanakaza kuendeleza ubabe kwa kukomalia sare kwa Simba kama mzunguko wa kwanza.

Lakini jambo la Pili litakuwa ni kuhakikisha wanachomoka mkiani mwa ligi kwani wako nafasi ya 15 kati ya timu 16.



BATTLE YA UFUNGAJI
Ndugu mtembeleaji wa MAHENGA BLOG Ukiangalia katika LIST ya wafungaji wanaoongoza Kichuya na Msuva wanalingana mabao na jana Msuva hakufanikiwa Kufunga.

Hivyo kichuya ataingia akiwa na njaa ya Kufunga ili ampite Msuva na Kumuogopesha Amis Tambwe anayekuja Nyuma ya Msuva na Kichuya akiwa na Goli 8 ilihali wao wana 9.
Ila Utamu Huu wa Leo unanogeshwa na Kipa anayekumbuka kuwa ndiye aliyewabania mpaka kutoa sare Said Kipao..

Chapisha Maoni

0 Maoni