Waliwa na mamba kwa ukosefu wa maji huko Ludewa

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa Dkt. Suzan Kolimba, akisikiliza kero za wananchi katika jimbo lake.




Wakazi wa Kijiji cha Luhuhu Wilayani Ludewa Mkoani Njombe, wamelalamikia uwepo wa mamba katika mto Ruhuhu wanaokula watu wanaokwenda kuchota maji katika mto huo.

Wakitoa malalamiko hayo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa Dkt. Suzan Kolimba, wamesema ukosefu wa maji safi na salama ndiyo sababi inayowafanya wakazi hao kutegemea maji ya mto huo ambao una mamba wanaokula watu.

Wananchi hao wameongeza kuwa licha ya kutegemea maji hayo kwa matumizi ya nyumbani lakini pia maji hayo si safi na salama hivyo wananchi wengi hukumbwa na magonjwa mbalimbali kutokana na matumizi ya maji hayo ikiwemo ugonjwa wa kuhara.


Akijibu Malalamiko hayo Naibu Waziri huyo Suzan Kolimba ameahidi kuwajengea kisima wakazi hao ambacho kitapunguza tatizo la maji kijijini hapo wakati serikali inaendela kutafuta suluhu ya kudumu ya kumaliza tatizo la maji katika eneo hilo.

Chapisha Maoni

0 Maoni