Mwakyembe Awapeleka Serengeti Boys Kucheza Everton ya Uingereza..


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe amesema ataviomba vilabu vingine vya nje viwachukue wachezaji wa timu ya taifa ya wenye umri chini ya miaka 17 wakapate uzoefu na kukuza vipaji.

“Nimeomba (Everton FC) wachukue vijana wawili kwenye vituo vyao vya kukuza soka la vijana, wamelipokea. Nataka kuona miaka michache ijayo tunakuwa na wachezaji wengi katika anga ya kimataifa,” amesema.

Pia Waziri Mwakyembe amesema ataendelea kuikumbusha klabu hiyo mara kwa mara ili kutimiza lengo hilo na kusisitiza kuwa kuna haja ya kuwatafutia wachezaji hao vituo vya soka vya kimataifa wakapate uzoefu wakuze vipaji baada ya kung’ara kwenye michuano ya Afrika nchini Gabon.

Chapisha Maoni

0 Maoni