Pele amponda mchezaji wa Juventus na timu ya taifa ya Argentina

GWIJI wa Brazil, Pele amesema ni kichekesho kumuita mshambuliaji wa Juventus na Argentina, Paulo Dybala ni Diego Maradona mpya.


Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa sasa ni mmoja wacheza gumzo kubwa Ulaya wenye umri mdogo baada ya kujiunga na Kibibi Kizee cha Turin kutoka Palermo mwaka 2015.

Dybala amefunga mabao 30 kwa misimu yake miwili ya kucheza Serie A, akishinda mataji katika misimu yote pamoja na kuisaidia timu hiyo kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Pamoja na hayo, vigogo hao wa Italia walisambaratishwa na Real Madrid mjini Cardiff kwa kufungwa 4-1 huku mashabiki wakimponda kinda huyo baada ya kucheza ovyo.

Na akatawala kwenye midomo ya watu baada ya kucheza ovyo pia jana licha ya Argentina kushinda 1-0 dhidi ya Brazil.

"Si mzuri kama watu wanavyosema,"amesema mshindi huyo wa Kombe la Dunia mara tatu.
"Wanasema atakuwa Maradona mwingine, lakini kitu pekee anachofanana na naye ni kutumia mguu wa kushoto tu,"amesema Pele.

Chapisha Maoni

0 Maoni