Mbunge wa Iringa
mjini (CHADEMA) Mchungaji Peter Msigwa amewapa rai wasomi wa vyuo vikuu nchini
ikiwa ni pamoja na chuo
kikuu cha Dodoma kuwa, waache kuiga wasomi ambao wamekuwa wakiitumia elimu yao pasi na kuiendeleza nchi, bali kunyume chake wamekuwa wanasiasa wasio na tija kwa taifa.
kikuu cha Dodoma kuwa, waache kuiga wasomi ambao wamekuwa wakiitumia elimu yao pasi na kuiendeleza nchi, bali kunyume chake wamekuwa wanasiasa wasio na tija kwa taifa.
Mchungaji Msigwa
ameyasema hayo katika kongamano la BAVICHA na CHASO katika ukumbi wa African
Dream mjini Dodoma, kongamano ambalo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali toka
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambapo mgeni rasmi aliyehudhuria
kongamano hilo ni Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA.
Katika rai yake,
Mchungaji Msigwa amewataka wanafunzi kuwa makini katika elimu yao na kuifanya
iwe na tija kwa taifa na si ‘mediocres’.
“mimi huwa siamini
katika midahalo ya wasomi wa vyuo vikuu na huwa siamini maprofesa kama kina Shivji…elimu
kama ya kina polepole mimi naiita, academic prostituition”. Amesema Mchungaji
Msigwa.
Katika hatua
nyingine, Mch. Msigwa ametoa maana ya neno BUNGE kuwa ni mkutano wa hadhara wa
wananchi. Tafsiri hii imekuja baada ya Mch. Msigwa kuitaka serikali ioneshe
moja kwa moja vikao vya bunge ili wananchi waone nin kinaendelea kwa
wawakilishi wao waliowatuma wkuwawakilisha.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA