Mbunge wa Jimbo la
Tarime Kijijini ambaye pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema
(BAVICHA), Mhe. John Heche aikosoa serikali ya awamu ya tano kwa kile
wanachodai ni utumbuaji majipu.
Mhe. Heche
ameyasema hayo katika ukumbi wa African Dream mjini Dodoma kwenye kongamano la
BAVICHA na CHASO ambalo pia limehudhuriwa na Viongozi wa CHADEMA na CUF
leo
tarehe 23 mwezi huu.
“Magufuli anacheza
na freedom ya nchi”. Amesema Heche. Katika hatua nyingine pia, Heche
ameitabiria serikali ya Magufuli kushindwa vibaya kutokana na kile
alichokilejelea kilichowahi kutokea kwenye serikali ya awamu ya nne ya Dr J.M.
Kikwete ambayo pia iliingia kwa mbwembwe na hatimaye taifa kugubikwa na ufisadi
wa kupindukia.
Pamoja na mengine,
Mhe. Heche amekizungumzia pia kile alichokidai kuwa rais hagusiki na
haambiliki. “ukimgusa magufuli, you are an enemy”. Amesema Heche.
Lakini pia, Mhe
Heche amezungumzia kuhusu Rais J.P.Magufuli kujitungia Bajeti na matumizi yake
mwenyewe na kuacha kile kilichojadiliwa bungeni. “Rais Magufuli katunga
matumizi yake na kuacha yaliyojadiliwa na bunge wakati posho za wabunge
zinaliwa kila siku ni tatizo”. Amesema Mhe. Heche.
Katika hatua
nyingine pia, Mhe Heche ameikosoa pia serikali kujitangaza kutaka kuanzisha
viwanda wakati serikali haijui viwanda hivyo vitazalisha nini na umeme wa
kuendesha viwanda hivyo bado unasuasua. “Je, kuna power ya kuviendesha viwanda
hivyo, au vitaendeshwa kwa power bank”. Amesema Mhe. Heche.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA