Akitangaza
maadhimio hayo katika kongamano lililofanyika katika ukumbi wa African Dream
ulioko mjini Dodoma leo tarehe 23 akiahirisha kongamano hilo, Katibu Mkuu wa vijana
na katibu Mwenezi Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe.
Edward Julius ameyatoa mapendekezo hayo na kutoa rai kwa vijana kutonunulika
kwa urahisi na chama tawala. Mapendekezo hayo pia yameungwa mkono na Umoja wa
Wanafunzi Chadema (CHASO) kama maridhiriano ya
nini kifanyike. Makubaliano hayo
matano ni kama ifuatavyo;
1. 1. Serikali
isiingilie mihimili mingine ikiwa ni pamoja na Bunge na hivyo vikao vya Bunge
vioneshwe moja kwa moja na Shirika la utangazaji la taifa (TBC).
2. 2 Kueneza
chachu hii nchi nzima kwa kujitolea na hivyo kutoa rai kwa vyombo vya ulinzi na
usalama kutowanyima haki yao ya msingi ya makusanyiko ya hadhaara,
3. 3 Serikali
iongoze kwa kufuata sharia na kanuni za nchi zilizoainishwa kwenye katiba ya
jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na kutaka katiba mpya itolewe.
4. 4 Kuendesha
harakati za kudai mabadiliko kwa kujitolea.
5. 5 Serikali
isipotenda haki, basi haki itapatikana barabarani-maandamano.
Pamoja na
mapendekezo hayo, Mh. Julius ametoa pia wito kwa vijana kufanya kazi kwa
kujitolea na bila uoga wa aina yoyote.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA