Mbunge wa Ukonga,
Mhe. Mwita Waitara (CHADEMA) aitolea macho serikali ya awamu ya tano chini ya
Dkt. J.P. Magufuli kuwa, kama iliona shirika la utangazaji la taifa (TBC)
linagharimu, basi wavipe uhuru vyombo binafsi vya habari ikiwa ni pamoja na ITV
na AZAM virushe matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge.
Mhe. Waitara
amesema, kwa kuwa vyombo binafsi vya utangazaji habari kama ITV na AZAM
havijawahi kuomba hela serikalini, basi serikali iviruhusu vyombo hivyo ili
virushe matangazo moja kwa moja ili kuwaendea haki
wananchi juu ya haki yao ya
msingi ya kupata tarifa.
“…wanaondoa
taarifa ili wananchi wasipate maarifa kama waliyonayo…” amesema Mhe. Waitara.
Katika hatua
nyingine, Mhe. Waitara amewataka vijana kushughulika na utoaji elimu katika
majimbo ya CCM ili wananchi wajue nini wawakilishi wao wa CCM wanawafanyia.
Kauli hii ameitoa kwenye kongamano la vijana lililofanyika leo katika ukumbi wa
African Dream, mjini Dodoma leo tarehe 23 aprili.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA