USICHOKIJUA KUHUSU TANZANIA: KUMBE MASHOGA WANA 'NGO' NA WADHAMINI KUTOKA NJE.

Labda tu niseme kwamba, suala la ushoga binafsi nimekuwa nikilishangaa sana na kutoliamini amini kama Tanzania linaweza kukubalika licha ya kuwa na aibu na fedheha kubwa kwa taifa teule kama hili. Nimeiangalia kwa masikitiko makubwa sana 'interview' ya Zamaradi wa Clouds na shoga maarufu kwa jina la 'kaoge', kiukweli pamoja na kuwa ni mahojiano ambayo kwa namna moja ama nyingine ni kuwaelimisha wazazi namna ya kuwakinga watoto wao na janga hili la kishetani kabisa, lakini tu pamoja na hayo ni kulidhalilisha taifa kwa kiwango cha hali ya juu sana kwani ni kitendo ambacho hadi sasa kimekuwa katika kizungumkuti na kigugumizi kikubwa kwa Tanzania na watanzania. TIZAMA MAHOJIANO HAYA HAPA

Ikumbukwe tu kwamba, suala hili kipindi cha nyuma liliwahi
kuleta vuguvugu na fununu anuai kuenea kuwa Tanzania yatakiwa kukubali ushoga ili kuendelea kupata misaada toka kwa mataifa yaliyoendelea, na kwa bahati mbaya sana kwangu, wala sikujua limeishia wapi, lakini tu nilichoishia kukiona ni nchini Uganda kipindi nikiwa shule mwaka juzi kipindi Rais Museveni alikemea suala hilo na kusema nchi yake haiko tayari kukubaliana na ushoga hata kidogo, na amri kali ilitolewa na rais huyo kuwa wote wanaoshiriki biashara hiyo ya aibu wakamatwe mara moja; sakata ambalo liliwakumba hadi wavaa vimini kwa madada. Kwa Tanzania hali ilikuwa tofauti, labda kama kuna msomaji wa makala yangu anaweza kunisaidia ni lini serikali iliwahi kuzungumzia suala hili la aibu kiasi hiki, kiukweli mimi kama mtanzania wa kawaida limenipa tafsiri mpya na hasi kwa taifa langu pendwa.

Ikumbukwe kwamba, Mwl Nyerere mwenyewe aliwahi kulizungumzia sakata hili akiwa nchini ujerumani alipohojiwa na mwandishi Hubert Fichte juu ya ushoga, alichojibu ni kwamba, ushoga ni kinyume cha asili ya kiafrika, hivyo shoga yoyote hatopata ulinzi wa aina yoyote hapa nchini.

In an interview with Hubert Fichte from Frankfurter Rundschau, Nyerere commented that homosexuality was alien to Africa and therefore homosexuals cannot be defended against discrimination. (Source: wikipaedia)

kwa kuwa alichokijibu kiliwagusa na kiligusa matakwa yao, chapisho hilo walilitoa.


Moja ya NGO ambayo shoga huyo aliyoitaja ni kwamba ipo Muhimbili na huwa wanaenda pale na kupewa vilainishi kwa ajili ya kuzuia michubuko wakati wa tendo. NGO hii imenipa swali ambalo mpaka naandika makala hii sijapata jibu sahihi, kama Muhimbili ni sehemu muhimu kwa serikali, je  ni kweli kwamba haitambui kuwepo kwa NGO hii na hawa watoa vilainishi?

Iliwahi kutokea pia Shinyanga, ambapo madiwani waliwahi kukaa kikao kuzungumzia juu ya huduma kama hizi ikiwa ni pamoja na kuwapa vilainishi mashoga; mjadala ambayo ulizua  tafaruki kubwa na kusababisha madiwani wa CHADEMA kususia kikao hicho kwa madai ya kuwa hawakuwa tayari kuunga mkono dhambi ile. Nikafikiri kwa akili yangu finyu kuwa mgogoro huo umefikisha ujumbe kwa serikali kuwa watanzania weneye nia na mapenzi mema na Tanzania hawakitaki kikombe hiki cha laana, lakini cha kushangaza kumbe ujumbe ulikomea tu IBINZAMATA, wala haukusafiri.

Hali ishakuwa mbaya kwa sasa, na wala sitaki kuzungumzia tafsiri ya ukimya wa serikali yangu pendwa, ila tu niseme kwamba, wantanzania kama kweli tunaamini Mungu mmoja na tunaamini kwa dhati ya mioyo yetu, hatuna haja kupiga vita vikali sana vitendo na biashara hii ya aibu. Niliwahi kulipigia kelele sana suala hili kwenye media, hasa DW  ikiwa ni pamoja na biashara ya kujiuza, lakini cha ajabu wahusika wanakamatwa saa moja jioni, kisha wanaachiwa saa mbili usiku na defender za vyombo vya ulinzi vikipita bila hata kujali tena, labda nikuulize msomaji wangu, unapata tafsiri gani? Sitaki kufika huko, ila tu kitendo cha mashoga kwa sasa kufikia hatua kutumia media za ndani na kujitangaza hadharani ni hatua nyingine ambayo ni fedheha kubwa kwa taifa na watanzania kwa ujumla. Isiwe chanzo misaada tukauza utu wetu na amali mbele za Mola wetu, nitoe wito kwa watanzania wa kweli kupinga vikali suala hili.

Chapisha Maoni

0 Maoni