Siku
moja baada ya mkuu wa mkoa wa Singida kufuta amri halali ya mkuu wa
wilaya ya Manyoni ya kuchangia shughuli za maendeleo na inayo wataka
wakazi wote wenye umri wa miaka kumina nane kuchangia shililingi elfu
kumina tano kwa mwaka,mkuu wa wilaya ya Manyoni naye amefuta rasmi amri
yake aliyoitoa Septemba sita mwaka huu .
Akiongea na waandishi wa habari mkuu wa wilaya ya Manyoni Bwana Geofrey
Mwambe amesema amri hiyo ambayo ilitolewa mwaka 2013 na mkuu wa wilaya
aliye kuwepo awali na yeye kuamua kuitekeleza,ameifuta rasmi baada ya
agizo la mkuu wa mkoa wa Singida kufuta amri hiyo.
Katika hatua nyingi Bwana Mwambe amesema taarifa zilizotolewa katika
mitandao ya kijamii ni uzushi na yeye na wakurugenzi wake hawajawahi
kupokea malalamiko ya mtu kulazimishwa kuchangia shuguli za maendeleo au
kupewa adhabu ya kufungwa.
Octoba 21 mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Methew Mtigumwe alitoa
taarifa kwa vyombo vya habari ya kumwagiza mkuu wa wilaya ya Manyoni
Bwana Geoffrey Mwambe kufuta amri inayo husu wakazi wa wilaya ya
Manyoni kuchangia pesa kwa ajili ya shuguli za maendeleo.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA