Umekwama na ndoto zako zinafifia? Makala hii
inakuhusu!
Maisha yana changamoto nyingi sana ambazo kamwe
huwezi kuzikwepa. Ukikubali changamoto hizo zikuzuie kufikia malengo yako
uliyojiwekea, hujipendi na huna tamaa ya
kufanikiwa katika maisha yako!
Kwa nini nasema hujipendi na huna tamaa ya kutaka
kufanikiwa katika maisha yako, nataka kuzungumza na wale ndugu zangu ambao
wamejikuta wakikwama katika mambo yao, kufilisika na hatimaye ndoto zao za
mafanikio kuyeyuka. it’s okay ni hali ya kawaida katika maisha jambo kama hilo
kutokea kwani wewe sio mtu wa kwanza kutokewa na hali kama hiyo. Sasa hebu
elekeza akili na mawazo yako hapa kwani naamini hutaondoka kama ulivyokuwa
kabla hujasoma Makala hii. Tiba kubwa ya matatizo yanayofanana na hayo ni
kukubali na kuanza upya na kukitafuta tena kilele cha mafanikio. Katika maisha
kuna wakati unapitia hatua mbalimbali za mafanikio. Lakini pia, naweza
ukajikuta umepoteza vitu vyote na kurudi kama zamani au Zaidi, Hayo ndio
maisha. Hata kama umepoteza kila kitu umebaki na afya yako ikiwa imara, shukuru
sana kwani huo ndyo mtaji pekee na ushindi mkubwa uliobaki nao. Inawezekana
kuanza upya, kuanguka kibiashara siyo mwisho wa maisha, kupoteza ulichokuwa
nacho siyo mwisho wa kila kitu. Tayari imeshatokea, huwezi kubadili hilo. Sawa
umepata hasara, unadhani huo ndio mwisho wa maisha yako? Hapana! Maisha lazima
yaendelee cha msingi hapo ni kukubaliana na matokeo na kukaa chini na kutuliza
akili. Kama kuna mahala umejikwaa na kuanguka, nyanyuka haaraka na uendelee na
safari. Kamwe usipaangalie mahala ulipojikwaa. Hapakuhusu tena, achana napo.
Songa mbele na mapambano ya maisha. Kuwa tayari kuanza upya. Ikifika mahali
huoni njia basi itengeneze mwenyewe. Pia kumbuka hutakiwi kufikiria sana
historia yako ya nyuma, mafanikio hayako nyuma bali mbele unakoelekea. Achana
na historia mbaya ya huko nyuma, hichi=o ulichokipoteza unaweza ukakirejesha
Zaidi ya hicho, hayo ndio maisha. Kama njia ya kwanza imeshindwa kukufikisha
unapotakaa kwenda, ni wajibu wako sasa kutengeneza njia nyingine.
Mwanasaikologia mmoja aliwahi kusema “kwenye kutafuta mafanikio unapokosa njia,
basi tengeneza njia”. Usiruhusu maisha yakuongoze/yakuendeshe, bali maisha
yaongoze wewe. Mwandishi mmoja wa vitabu aitwaye Michael Gian aliwahi kupata
ajali mbaya ya ndege . akapoteza miguu
yote na kupooza kuanzia shingoni hadi kiunoni! Akafilisika baada ya kuingia
madeni makubwa wakati wa kutibu majeraha na afya kwa ujumla. Lakini jamaa huyo
alianza upya kwa kuwatia watu moyo. Akawa anazungumza akiwa kwenye kiti cha
kusukuma cha matairi. Akihamasisha watu kujikomboa na umaskini. Leo hii ni
bilionea na anamiliki viwanda na ndege kadhaa kama usafiri wake binafsi. Hayo
ndio maisha na mtu huyu akufanye wewe uamini kwamba, ukianguka bado unaweza
kusimama na ukafanya mambo makubwa Zaidi. Yaani unaweza kupata mafanikio Zaidi
hata ya uliyokuwa nayo hapo awali. Wakati mwingine Mungu humfilisi mtu kwa
makusudi pengine mtu ajifunze kuishi kuanzia chini kwenda juu.
Hivyo basi huna sababu ya kujiona mnyonge na kuhisi
safari yako ya kuelekea kwenye mafanikio imeishia njiani, huo uwe mwanza wa
kupambana na trust me hakuna linaloshindikana ukiamua kupambana.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA