Zanzibar.
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuna njama za kumkamata na kumpulizia sumu itakayomuua taratibu.
Maalim Seif aliyezaliwa Oktoba 22, 1943 katika Kijiji cha Nyali
wilayani Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, amesema hayo wakati akisherehekea
siku yake ya kuzaliwa.
Mwanasiasa huyo mkongwe ametoa tuhuma hizo juzi mbele ya wajumbe wa
Kamati ya Utendaji, Baraza Kuu, viongozi, watendaji na wafuasi wa CUF.
“Kwa taarifa za kuaminika, zipo njama za kunikamata, wanipeleke Dar es
Salaam, kama walivyowafanyia masheikh. Waniweke katika chumba maalumu
kidogo, kisha wanipulizie dawa hatimaye afya yangu izoroteshe afya
taratibu na mwishowe nifariki dunia,” amedai Maalim Seif bila ya kutaja
wanaotaka kumkamata.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA