MAKONDA: WANAFUNZI WATAKAOFANYA VIZURI KIDATO CHA NNE NA CHA SITA WATAPEWA MOTISHA.


Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam ametangaza neema kwa wanafunzi watakaofanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho wa kidato cha nne na sita. Makonda ameyasema hayo katika mahari ya shule moja huku akiweka wazi kuwa, kwa wanafunzi watatu
wa kidato cha sita watakaofanya vizuri watapewa pesa taslimu kiasi cha shilingi milioni 2.

Wanafunzi watakaofanya vizuri mtihani wa kidato cha nne watapewa fursa ya kuchagua shule yoyote nzuri iliyopo hapa Tanzania na watasomeshwa.

Makonda pia ametoa dau kwa walimu watakaofanya vizuri katika masomo yao kuwa, kila mwalimu atapewa nafasi ya yeye na familia yake kutembelea mbuga za wanyama kwa gharama zake-mkuu wa mkoa.

Chapisha Maoni

0 Maoni