Wiki iliyopita Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Maarufu kama Msukuma
alimvua ukuu wa shule ya Sekondari Kasamwa bwana Denissi Otieno kwa
kukataa kuwaruhusu wanafunzi wa CCM walioanzisha MAGUFULI CLUB chini ya
mwalimu mwanaccm shuleni kinyume na sheria na kanuni Za utumishi wa
umma
.
Wanafunzi wa CCM wanachama wa MAGUFULI CLUB shule ya Sekondari Kasamwa
walikua na mahafali shuleni hapo maana walikua wanafanya siasa shuleni
bila bughugha ingawa mkuu wa shule alikua akigombana Sana na Mwalim
mlezi wa wanafunzi wa MAGUFULI club ambaye ni rafiki mkubwa Sana wa
Msukuma na anatoka kijiji kimoja na Magufuli Chato.
Mkuu wa shule Denissi Otieno alifikia kikomo cha UVUMILIVU (Zero
tolerance) baada ya Mwalim huyo mwanaccm kutangaza assemble kwamba
kidato cha nne wote wanachama wa MAGUFULI club wavae nguo za Ccm kwa
ajili ya mahafali ndipo Mkuu wa shule akagoma jambo Hilo kufanyika
shuleni kinyume na kanuni na sheria za utumishi wa umma. Kanuni Za
utumishi wa umma to leo la 2009 (public service standing order, 2009)
kanuni namba F21 (a) - (h) inakataza kabisa mambo ya siasa kufanyika
eneo la Kazi na Muda wa Kazi.
Pia sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992 kifungu cha 12(2)
kimekataza kabisa shughuli za kisiasa kufanyika shuleni na taasisi
nyingine za umma ikiwa ni Pamoja na kuanzisha tawi la chama, Umoja wa
wanawake au Baraza La wanawake, vijana nk.
Mkuu wa shule alipokua anatangaza kupinga wanafunzi kufanyia mahafali
shuleni, Mwalim mwanaccm aliirekodi speech ya mkuu wa shule na kumtumia
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Bwana msukuma, usalama wa taifa,
mkurugenzi mtendaji nk.
Msukuma aliamua kumvua uongozi wa ukuu wa shule Denissi Otieno na
kuagiza afisa elimu na mkurugenzi kumpatia Barua mwalimu huyo bila
kumuhamisha shule na kumpangia vipindi vya kufundisha.
CHANZO
jamiiforums
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA