Serikali imesitisha shughuli iliyokuwa ikiendeshwa na Mchungaji Getrude
Lwakatare ya kuwalipia faini wafungwa walioko magerezani hadi hapo
utaratibu mwingine utakapotolewa.
Mpango huo unaofanywa na Lwakatare kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa
Taifa wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema tayari umewezesha wafungwa 78
kutoka magerezani baada ya kuwalipia faini inayofikia Sh25 milioni.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Antonio Kilumbi alisema amepata
maelekezo ya kusitishwa kwa mpango huo kutoka ngazi ya juu ya jeshi
hilo.
Alisema wananchi wengine bado wanaweza kuwalipia faini hiyo ndugu zao.
Mrema alisema jana kuwa mpango huo ulilenga kupunguza msongamano
magerezani na kuipunguzia Serikali gharama za kuwahudumia wafungwa
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA