Hoteli ya Kifahari ya Arusha iitwayo Snow Crest itapigwa mnada mwezi huu
kwa mujibu wa tangazo lililotolewa kwenye gazeti. Tangazo hilo
lililotolewa na kampuni inayojulikana kama First World Investment Court
Brokers, limedai kuwa hoteli hiyo itapigwa mnada
Septemba 23, saa tano asubuhi.
Mwakilishi wa kampuni hiyo, Allan R Mollel ameiambia Bongo5 kuwa hoteli
hiyo ilipelekwa mahakamani na shirika la hifadhi ya jamii, NSSF kwa
kushindwa kuwalipa wafanyakazi
michango yao.
“Hiyo hoteli inauzwa kwasababu ya kesi iliyokuwa mahakamani ambayo
hoteli hiyo inadaiwa na NSSF michango ile ya wafanyakazi kwa maana
kwamba hiyo hoteli walikuwa
hawafikishi michango ya wafanyakazi NSSF. Kwahiyo NSSF wakafungua kesi
wameshinda na wakaomba kuuza hii hoteli ili kuweza kupata michango hiyo
ya wafanyakazi,” Mollel
ameiambia Bongo5.
Amedai kuwa NSSF inaidai hoteli hiyo shilingi milioni 442 ambazo ni
michango ya NSSF kwa wafanyakazi wake. Hata hivyo Mollel amesema
kisheria hoteli hiyo bado ina nafasi ya
kuzilipa fedha hizo kwa NSSF pamoja na gharama za dalali na wakaendelea kuwa na umiliki wa hoteli hiyo.
“Sasa hivi kilichoongezeka hapo ni gharama za dalali,” amesema. “Kama
wataweza kulipa fedha zote wanazodaiwa na NSSF, wakalipa na gharama za
dalali, mambo yatakuwa yamefika mwisho.”
Ni vyema mashirika na makampuni mengine yakajifunza kwa yanayo endelea
kwa hii hotel kupeleka michango ya wanachama mahala husika ni muhimu
sana..
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA