Mfuko wa
Singita Grumeti umeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuboresha hali ya elimu katika Wilaya za Serengeti na
Bunda.
Hii imedhihirika kwenye halfa ya kukabidhi madawati 500 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara
Dk. Charles Mlingwa
ili kupunguza uhaba wa madawati katika Wilaya hizo. Aidha Grumeti
wamekabidhi nyumba ya kuishi mwalimu iliyojengwa katika Shule ya Msingi
Makundusi.
“Tuko hapa kukabidhi madawati haya 500 yenye thamani ya Tshs Milioni 112
kwa Wilaya za Serengeti na Bunda pamoja na nyumba hii yenye thamani ya
[E1] Milioni 86” alisema
Richard Ndaskoi ambae ni Mkuu wa Huduma za Jamii toka Mfuko wa Singinta Grumeti.
Akipokea misaada hiyo, Dk. Mlingwa alisema “Nawashukuru Singita Grumeti
kwa Msaada huu wa madawati pamoja na nyumba hakika mchango wenu katika
Mkoa wa Mara unaoneka” Dk Mlingwa amewataka wawekezaji wengine katika
Mkoa wa Mara kuchangia madawati katika Wilaya za Serengeti na Bunda
kwani bado zina uhaba wa madawati.
Aidha Dk. Mlingwa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kwa
kuwa na mahusiano mazuri na wawekezaji waliopo katika Wilaya hiyo
“Tukiwawekea mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao hata wananchi pia
watanufaika na uwepo wa wawekezaji hawa” alisema Dk. Mlingwa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Serengeti,
Nurdin Babu pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bunda,
Lydia Bupilipili
wote kwa nyakati tofauti wameushukuru Mfuko wa Singita Grumeti kwa
msaada huo wa madawati na kuuomba mfuko huo kuendelea kuchangia katika
shughuli za maendeleo katika Wilaya za Serengeti na Bunda. “Wilaya hii
ina wawekezaji wengi lakini wamekuwa nyuma katika kuchangia shughuli za
maendeleo, nawapongeza kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia jamii
inayowazunguka pamoja na kuchangia katika maendeleo ya Wilaya ya
Serengeti” alisema Nurdin Babu.
Aidha Bi. Bupilipili ameuomba Mfuko huo kuanzisha kampeni maalumu ya
kuongeza kiwango cha ufaulu kwa watoto wa kike kwa shule za sekondari
Wilayani Bunda.
Singita Grumeti wamekuwa wawekezaji wenye tija kwa wananchi wa Wilaya za
Serengeti na Bunda licha ya kuwa mstari wa mbele kuchangia katika
shughuli za maendeleo, kampuni hiyo pia imekuwa ikitoa ajira kwa wakazi
toka wilaya hizo mbili pamoja na kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi
toka wilaya hizo.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA