Kamati ya fedha za serikali (PAC) imemuagiza CAG na BOT kukagua
ubadhirifu wa riba/faida ya akaunti za muda maalum kiasi cha shilingi
Bilioni 440 za Mamlaka ya bandari, zilizowekwa katika benki zifuatazo
CRDB,NBC,NMB na Standerd Charterd bank.
-Kiasi hicho cha 440 Bil. Kimewekwa katika fixed deposit ya mwaka na
kuzaa Bilioni 17 tu sawa na wastani wa asilimia 4 kwa mwaka.
Uhalisia kwa riba za kawaida kwa ‘fixed deposit’ chini ya milioni 100 ni
asilimia 8 mpaka 10, lakini pesa zinapoongezeka huongezeka hadi kufikia
asilimia 15 ili benki ivutie amana zaidi ambazo kimsingi huziwekeza
kupitia mikopo na kununua hati fungani za serikali. Tuseme, benki zitoe
riba ya asilimia 13 kwenye amana za Bilioni 440 Bandari ingepata si
chini ya shilingi Bilioni 57.2 kabla ya kodi (51.7 Bilioni baada ya
kodi), kwa hiyo serikali (wananchi wameibiwa takribani Bilioni 40 kwa mwaka 2014/2015.
Mbaya zaidi pesa hizi bilioni 440 zinapokuwa kwenye mabenki ya biashara,
serikikali hukopesha pesa hizi (pesa zake) kupitia ‘treasury
bills’/hati fungani kwa riba ya hadi asilimia 15 kwa mwaka. Hivyo
wananchi hilipa mabenki haya riba ya hadi shilingi Bilioni 66 kwa hela
ambayo ni ya kwa wenyewe. Sasa ukijimlisha hasara kamili kwa mwaka
utakuja wananchi/serikali inapata hasara ya Bilioni 66+ Billioni 40
(riba inayopunjwa na benki kwa pesa zilizoko kwenye ‘fixed deposit’= 106
Bilioni, sasa chukua mashirika mengine kama EWURA, TANAPA, SUMATRA,na
mamaka mbalimbali utagundua ni kiasi gani wananchi wanaibiwa kupitia
mabenki kila mwaka. Hapa huhitaji kuambiwa uzalendo wa JPM na Waziri wa
Fedha Dr. Mpango.
Jinsi gani wizi huu unatekelezwa;
Maafisa wa benki (treasury/dealers/CEOs) na maafisa wa bandari huungana
kufanya wizi huu kwa makusudi. Benki za biashara hutenga fungu/kasma
maalumu kwa ajili ya kuwalipa maafisa wa mashirika ya umma ambao
watafanikisha wao kupata fedha hizi ili kufikia malengo yao kibiashara.
Kuna sera maalum kabisa, unakuta asilimia 10 ya faida (57.2) ni
‘commision’ ya maafisa wa serikali na asimia 10 nyingine hulipwa kama
‘bonus’ kwa maafisa wa benki kwa kufikia malengo ya biashara (target);
kwa hiyo hela hizi kwa benki hutoka kama matumizi ya kawaida na wanajua
jinsi wanavyogawia maafisa wa serikali. Ni ngumu kwa benki inayofuata
maadili kupata biashara hii, hata uwe na maafisa masiko wazuri vipi,
hata benki yako itoe ofa ya interest rate ya 15 kwa fixed deposit kamwe
hutapata amana hizo huu ni mtandao wa wizi.
Vile vile maafisa hawa wa benki huungana na maafisa wa serikali kuibia
serikali kupitia mauzo na manunuzi ya fedha za kigeni. Kanuni ni ile
ile. Ikiwa serikali inataka kununua fedha za kigeni, bei hutolewa ya juu
mfano badala ya kuuza dola moja kwa shilingi 2100 serikali inauziwa
dola moja kwa shilingi 2200, fikiria kama serikali inafanya manunuzi ya
dola milioni 20, huishia kupata hasara ya shilingi milioni 200.
Baadhi ya wati sasa wataelewa ni kwanini baadhi ya wakuu wa baadhi ya
benki na mashirika ya umma walipiga kelele pale Raisi alipoamuru fedha
zote za taasisi za umma zirejeshwe benki kuu. Si kwamba walimaanisha,
hapana walijua mwisho wao umefika. ‘Performance’ yao halisi itajulikana
kwani walitumia fedha za rushwa kufanya biashara na kupata faida kubwa.
Benki nyingi zinapitia uhalisia,zimekwama njia pekee iliyobaki ni kubuni
mbinu mpya haswa bidhaa mpya kwa ajili ya wananchi na si kuvizia
matrilioni ya serikali. Serikali ni mteja na ana haki ya kuchagua mahala
pa kuweka fedha zake na kiutamaduni benki ya serikali ni Benki kuu si
benki za biashara.Hawa wote ni wateja wa mahakama ya mafisadi.
Mtandao huu una nguvu, umetumia ukwasi huu kuwalipa waandishi wa habari
kupotosha mengi ili kuficha ukweli. Nampongeza Raisi Dr.Magufuli,
hajakubali kugeuka jiwe,siku hata siku mambo yao yanaanikwa hadharani na
ripoti za CAG, ukweli haupendi kupuuzwa.Tunataka Tanzania Mpya.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA