Radio Free Africa kipindi cha michezo asubuhi hii wametangaza kifo cha
ghafla cha Bondia Thomas Mashali. Thomas ni bondia aliyeleta changamoto
kwenye gemu na kuifanya ichangamke.
Chanzo cha Kifo chake inadaiwa kuwa kimesababishwa na kipigo cha wananchi hapa maeneo ya Kimara.
=======
Mashali aliyezaliwa kwa jina Christopher Fabian Mashale aliuawa baada ya
kupigwa akiwa huko Kimara jijini Dar es Salaam. Inasemekana wakati
akinywa pombe, ulizuka ugomvi na mtu mmoja ambaye anadaiwa kupiga kelele
kusema Mashali ni mwizi na watu kuanza kumshambulia.
Ndugu zake wanadai kuwa walimkuta akivuja damu nyingi.
Taarifa zinadai kuwa alipelekwa katika hospitali ya Sinza Palestina
kabla ya kupelekwa Muhimbili ambako mauti ilimkuta. Inasemekana kuwa
hadi jioni alikuwa na bondia mwenzake, Francis Cheka.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA