1. Kwanza ningependa niwasalimie wapenzi na wanachama wa UKAWA kwa
ujumla wenu nashukuru kwa meseji zenu ambazo nimezipata ni 297,576 (laki
mbili tisini na saba elfu na mia tano sabini na sita). Ingawa
nimejitahidi kusoma nyingi, na Bado napitia zingine.
2. Na wengi wao wana lalamika mbona UKAWA (Chadema) hamchukui hatua kwa udhalimu na Visasi mnaotendewa?
3. Ila niwajibu hivi :-
Mnakumbuka Raisi wa zamani Laurent Gbagbo wa Ivory Coast alivyoshindwa
uchaguzi ili alilazimisha tume yao ya uchaguzi wamtangaze ameshinda
uchaguzi ule, Na tume ile kwa sababu ilikuwa sio huru, iliteuliwa na na
yeye, na waliogopa kutenguliwa kipindi kile walimtangaza kuwa yeye
Laurent Gbagbo ni mshindi badala ya mshindi halali ambaye alikuwa
Alassane Ouattara na sasa ameshitakiwa Mahakama ya ICC, Kwa hiyo haya ni
mambo ya muda tu.
4. Mfano wa pili ni Samweli Doe wa Liberia ambaye baadaye alipinduliwa
na rafiki yake ambaye alikuwa na jeshi dogo lakini wananchi walimuunga
mkono kutokana na kupinga udhalimu uliokuwa ukitendwa na watu wake
Samweli Doe.
5. Ila sisi Upinzani hatupendi tuingie kwenye Vurugu za kuhatarisha
Amani ya nchi ingawa tuna bambikizwa na kesi za uchochezi kila kukicha
na tunasikia tu kuwa wao wanapokea amri kutoka Juu kwa hiyo wanatimiza
amri hiyo.
6. Ila niwaambie neno moja tu kutokana na utafiti huu Dikteta anajimaliza mwenyewe, huku wapiga vigelegele wake wakimpoteza.
7. Napenda mfahamu pia kuwa sio watu wote waliopo kwenye system hiyo ya
kidikteta wanafurahia matendo hayo yote tunayofanyiwa , na wanatupatia
taarifa ya mambo wanayotaka kutufanyia.
8. Mambo haya ni mazito na Msikimbile kuwa na hasira, kwani hasira hasara.
9. Madikteta wengi huwa wana chuki na visasi moyoni mwao na vitu
wanavyofanya huwa wanafanya kwa malengo yao maalum na kupanga safu yao
uongozi kwa malengo maalumu mfano:-
10. Wanaweza kuweka kikwazo Fulani fulani au kuleta kitu fulani ili
vurugu ifanyike ili wao wapate sababu au kisingizio cha kumpata mtu
Fulani ili kulinda maslahi yao, kama vile kumkamata mtu na kumtia
kizuizini ili lengo Fulani litimie kama ushindi wa uchaguzi, au
vinginevyo, na pia kuvipunguzia nguvu vyama fulani au kuviua nadhani
mmeona kwa kupitia kwa Bwana Yule.
11. Inafahamika wazi kabisa kwao kuwa watu wameshajua mambo yao mengi na
Madikteta wanajua kuwa hawakuingia madarakani kwa ushindi halali, hali
inayowapa presha na kufanya mambo kwa kukurupuka ili kuokoa jahazi, pia
kukwamisha maendeleo kwenye Miradi au mipango kwenye maeneo ya
wapinzani.
12. Napenda niwasihi makamanda wote na wapenzi wa UKAWA tuwe na Busara
kwani Afrika tuko kwenye hali mbaya sana,na Tufahamu kuwe Dikteta
anjimaliza mwenyewe, ni swala la Muda tu.
13. Kuna Vilio kila kona na kila idara, na kwa mujibu wa utafiti Dikteta
atajimaliza mwenyewe kama wengine walivyojimaliza. Historia huwa
inajirudia.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA