Wakazi
wa Mji mdogo wa Himo wilayani Moshi wameshangazwa na kitendo cha Jeshi
la Polisi mkoani humo kutowachukulia hatua maofisa wake wawili
wanaohusishwa na mtandao wa wizi wa magari.
Maofisa hao wawili wanaotuhumiwa, mmoja anacheo cha Mrakibu wa Polisi
(ASP) na mwingine Koplo walikamatwa na magari matatu ambayo
waliyasafirisha hadi jijini Dar es Salaam.
Taarifa kutoka ndani ya Polisi zinaeleza kuwa maofisa hao walikamatwa na
kikosi kazi maalum kutoka Dar es Salaam tangu mwezi uliopita lakini
hadi leo hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.
Katika operesheni hiyo, mtuhumiwa mwingine ambaye ni raia alikamatwa
nyumbani kwa Koplo huyo akiwa na gari moja la wizi na vibao vya namba za
magari 70.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mtafungwa alipoulizwa na
gazeti la Mwananchi alikiri maofisa hao kukamatwa na magari hayo
akasema lakini mtu hawezi kupewa adhabu kabla ya kuthibitika kuwa
kafanya uhalifu.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA