Kuelekea
uchumi wa viwanda nchini, serikali imefanikiwa kufufua na kuanzisha
viwanda ambapo kwa sasa vinavyofanya kazi vipo zaidi ya 52,000. Sekta
hiyo pia imetajwa kuwa inatarajia kukuza uchumi wa watanzania asilimia
40.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles
Mwijage wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonesho ya
viwanda Tanzania yanayotarajiwa kufanyika katika viwanja vya sabasaba
jijini Dar es Salaam kuanzia Disemba 7 hadi 1, 2016.
“Kuelekea ujenzi wa uchumi wa viwanda, nilipewa maelekezo kufanya mambo
matatu, ikiwemo uhakikisha vilivyopo ambavyo vingi vilikuwa vinazalisha
chini ya kiwango vinaongeza uzalishaji, pili vilivyobinafsishwa ambavyo
havifanyi kazi vinafanya kazi na la mwisho nilipewa agizo la kuhakikisha
wekezaji wa ndani na nje ya wanakuja kuwekeza,” amesema na kuongeza.
“Katika kipindi cha mwaka mmoja tangu serikali hii iingie madarakani,
kuna viwanda 52,000 vinafanya kazi na kwamba asilimia 40 ya watanzania
uchumi wao utatokana na viwanda.”
Aidha, Mwijage amesema Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia
taasisi yake ya Mamlaka na Maendeleo ya Biashara Tanzania, imeandaa
maonesho yatakayokutanisha wadau wa sekta ya viwanda kwa lengo la
kutangaza pamoja na kujadili fursa za masoko ya ndani na nje ya nchi.
Amesema maonesho hayo pia yatatoa taswira ya juhudi za ujenzi wa viwanda katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA