Dar
es Salaam.
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umeingia kwenye jaribio
jingine, baada ya Wazanzibari 40,000 kufungua kesi mahakamani kupinga
uhalali wake.
Kesi hiyo ilifunguliwa jana katika Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki
(EACJ) na Rashid Salum Adiy kwa niaba ya wenzake 39,999, katika Masijala
ndogo ya mahakama hiyo iliyoko jijini Dar es Salaam.
Wadaiwa katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Chanzo: Mwananchi
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA