Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mwanza, Dk Anthon Dialo amesema sababu kubwa ya fedha za maendeleo kutotumwa kwa halmashauuri ni suala la elimu bure kutekelezwa nje ya bajeti.
Diallo, ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, amesema sababu nyingine ni Uchaguzi Mkuu uliopita na mchakato wa Katiba mpya ambao ulitumia fedha nyingi.
Mwenyekiti huyo amesema hayo baada ya mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Yanga Makaga kuiomba Serikali kuharakisha kutoa fedha za miradi ya maendeleo kwa kuwa hakuna hata mmoja ulioanza kutekelezwa.
Makaga ametoa kauli hiyo katika kikao cha wakuu wa idara kilichoitishwa na mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole kwa ajili ya kujadili uwajibikaji. “Kitendo hiki kinawafanya madiwani kuacha kufanya mikutano ya hadhara katika kata zao wakikwepa kuulizwa maswali ya miradi waliyoahidi,” amesema Makaga.
Kuanzia Julai hadi sasa halmashauri hiyo imepokea Sh45 milioni ambazo hazitoshi kutekeleza miradi iliyopo, hali inayosababisha wananchi wawalaumu watendaji kwa kushindwa kutimiza ahadi za Serikali.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA