Mvua
ya mawe ya barafu iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha kwa muda wa
dakika 20 imesababisha maafa makubwa kwa wananchi wa kitongoji cha
Kigambo kijiji cha Kasuro wilaya ya Ngara mkoani Kagera ambapo watoto
watatu wa familia moja wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na kuta za
nyumba, kaya 39 kukosa makazi huku mashamba na miti mikubwa ikisombwa na
maji.
Akithibitisha kutokea kwa maafa yaliyozikumba familia 39 mwenyekiti wa
kijiji cha Kasuro Bw.Peter Rusesa wakati akizungumza na ITV
iliyotembelea eneo hilo na kujionea hali halisi ya uhalibifu wa
mashamba, nyumba kuanguka na miti mikubwa kuvunjika amesema kuwa mvua
hiyo imesababisha madhara makubwa kwa jamii wakiwemo wazee.
Baadhi ya waathirika wameiambia ITV kuwa mvua hiyo imeanza kunyesha
majira ya saa tisa mchana huku maeneo mengine jua likiwaka hali
iliyowashangaza kwa maajabu ya kupata mvua katika kitongoji cha Kigambo
na kuwasababishia janga la kukosa makazi na mashamba ya Migomba ya ndizi
kuhalibika vibaya.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA