Kiwanda
cha Saruji cha Dangote huko Mtwara kimesitisha uzalishaji kutokana na
gharama kuelemewa na gharama za uendeshaji hivyo kuwaacha watumiaji wake
njia panda.
Hayo yalisemwa na mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho Harpeet Duggal
Walisema wapo na mazungumzo na serikali kuona namna ya kutatua changamoto hiyo
Mwezi uliopita mkurugenzi huyo alilalamika uamuzi wa serikali kupiga
marufuku kiwanda chake kuingiza makaa ya mawe kutoka Afrika Kusini na
kutakiwa kutumia ya Liganga ambayo alidai yapo chini ya kiwango na bei
ghali.
Pia alilalamikia shirika la maendeleo ya petroli TPDC kwa kushindwa
kuwauzia gesi kwa bei rahisi wakati inazalishwa mkoani Mtwara
Waziri Sospeter Muhongo alidai madai yao ya gharama kuwa juu ni ya uzushi.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA