RAIS
John Magufuli jana aliwapokea marais wawili, Edgar Lungu wa Zambia
aliyewasili kwa ziara ya kiserikali na Idriss Deby wa Chad aliyekuja
kikazi.
Tofauti
na Lungu ambaye ziara yake ilifahamika tangu wiki iliyopita, ujio wa
Rais wa Chad ulikuwa wa ghafla na hata serikali ilitoa taarifa ya ujio
wake jana saa chache kabla ya kuwasili nchini kiongozi huyo ambaye kwa
sasa ndiye Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).
Wote wawili baada ya kuwasili nchini walipigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride na ngoma za asili.
Licha
ya kupokelewa na Rais Magufuli, viongozi wengine waandamizi wa Serikali
pia walishiriki kwenye mapokezi ya viongozi hao. Rais Deby aliwasili
saa 8 mchana na kulakiwa na Rais Magufuli na Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa, mwenzake Lungu aliwasili saa 11.20 alasiri na kulakiwa na Rais
Magufuli na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
Ratiba ya ziara yao inaonesha kuwa kila mmoja atafanya mazungumzo Rais Magufuli katika Ikulu ya Dar es Salaam.
Shughuli za Lungu
Ratiba
ya Rais Lungu inaonesha leo asubuhi atatembelea ofisi za Mamlaka ya
Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kujionea shughuli mbalimbali
zinazotekelezwa na shirika hilo la ubia baina ya nchi hizo.
Baadaye
atazuru pia Shirika la Bomba la Mafuta la Tazama, ambapo atatembelea
mitambo ya kusukuma mafuta, pamoja na matangi ya kuhifadhi mafuta ya
Tazama vyote vilivyopo eneo la Kigamboni.
Baada
ya ziara hizo za asubuhi, Lungu na ujumbe wake watafanya mazungumzo
rasmi na Rais Magufuli, pamoja na Viongozi Waandamizi wa Serikali ya
Tanzania.
Mazungumzo
hayo yatafanyikia Ikulu kuanzia saa 5:00. Marais hao wawili pia
watashuhudia utiaji saini wa Makubaliano na Mikataba mbalimbali minne
(4) ya ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania kwa upande mmoja na
Serikali ya Zambia.
Taarifa
ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilifafanua
kuwa mikataba hiyo inahusu kuimarisha na kukuza zaidi uhusiano uliopo
baina ya nchi hizo. Katika ratiba hiyo, leo jioni Rais Lungu atahudhuria
dhifa ya kitaifa itakayoandaliwa kwa heshima yake na Rais Magufuli.
Dhifa hiyo itafanyika Ikulu kuanzia saa 12;30 jioni.
Aidha,
kesho Rais Lungu atatembelea Bandari ya Dar es Salaam ambapo atajionea
shughuli mbalimbali za upokeaji na upitishwaji wa mizigo bandarini hapo.
Baadaye
atafanya ziara fupi kwenye Kampuni ya kusafirisha mizigo inayomilikiwa
na Serikali ya Zambia inayojulikana kama Zamcargo, kisha ataelekea
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ambako ataagwa
rasmi na mwenyeji wake Rais Magufuli kurejea nchini kwake Zambia.
Katika
taarifa hiyo ya Mambo ya Nje inaeleza kuwa ziara ya Rais Lungu
inatarajiwa kutoa fursa ya kuzidisha uhusiano na kukuza ushirikiano ili
kuongeza ufanisi wa Reli ya Tazara ambayo ni mhimili na kiungo muhimu
katika ukuzaji wa uchumi wa Tanzania na Zambia, lakini pia na kwa nchi
nyingine majirani za ukanda wa kusini na kati mwa Afrika za Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Zimbabwe na Malawi.
Pia
eneo lingine litakuwa ni kukuza ushirikiano katika matumizi ya bomba la
Tazama ambalo lilijengwa mwaka 1968 kwa lengo la kutoa njia nafuu ya
kusafirisha mafuta ghafi kwenda nchini Zambia na hivyo kuiepusha nchi
hiyo na athari za kupanda kwa bei ya mafuta. Hata sasa umuhimu wa bomba
hilo bado upo.
Eneo
lingine litakuwa ni ushirikiano katika matumizi ya Bandari ya Dar es
Salaam ambayo kwa muda mrefu Zambia kama nchi ambayo haina bandari
imekuwa ikitumia Bandari ya Dar es Salaam kupitisha mizigo yake. Kwa
sababu za kiuchumi na za kihistoria, nchi hiyo imeendelea kuwa mdau
mkubwa katika matumizi ya bandari hiyo.
Rais Deby
Taarifa
iliyotolewa na serikali inaonesha Rais Deby ambaye ni Mwenyekiti wa
Umoja wa Afrika, atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Magufuli
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na watapata
fursa ya kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu
Ukanda wa Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika kwa ujumla.
Deby
amefuatana na mkewe, Hinda Deby, Moussa Faki Mahamat ambaye ni Waziri
wa Mambo ya Nje, Mtangamano wa Afrika, na Ushirikiano wa Kimataifa wa
Chad na viongozi wengine waandamizi wa Serikali ya Chad.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa
na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe Idriss Deby Itno mara baada
ya kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 27, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu akisalimiana na mabalozi
wanaowakilisha nchi mbalimbali za Afrika nchini mara tu baada ya
kupokewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Magufuli katika uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 27, 2016.
Tofauti na Lungu ambaye ziara yake ilifahamika tangu wiki iliyopita, ujio wa Rais wa Chad ulikuwa wa ghafla na hata serikali ilitoa taarifa ya ujio wake jana saa chache kabla ya kuwasili nchini kiongozi huyo ambaye kwa sasa ndiye Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa
na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe Idriss Deby Itno mara baada
ya kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 27, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu akisalimiana na mabalozi
wanaowakilisha nchi mbalimbali za Afrika nchini mara tu baada ya
kupokewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Magufuli katika uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 27, 2016.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA