Wakati tunaingia kwenye soko huria na kuanzishwa kwa sheria ya Banking
and Financial Institutions Act of 1991 nchini, National Bank of Commerce
(NBC) ilikuwa inahodhi 90% ya amana zote za kibiashara wakati
Cooperative & Rural Development Bank (CRDB) ilikuwa inahodhi 5% ya
deposits huku amana zilizobaki zikihodhiwa na People's Bank of Zanzibar
na Tanzania Housing Bank (THB)
.
Tanzania ya sasa ina mabenki na vyombo vya fedha zaidi ya 53 kwenye
uchumi ambao umeshikiliwa na matajiri wachache sana huku mamilioni ya
wananchi wengine ambao wengi wao zaidi ya 70% wanaishi vijijini wakiwa
hawana hata akaunti kwenye banki au vyombo vya fedha.
Kwa mujibu wa gazeti la The Citizen, Watanzania asilimia 17 tu ndio wana
akaunti kwenye haya mabenki. Ikumbukwe kuwa huwezi kupewa mkopo kama
huna bank account. Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi 2012, Tanzania
yenye watu 44,928,923 ina Watanzania karibia 3,820,000 ambao wana
akaunti kwenye mabenki nchini.
Financial Stability Report iliyotolewa na BOT inaonyesha zaidi ya 71% ya financial system's total assets ziko chini ya mabenki.
Cha kushangaza zaidi, sheria zilizopigiwa chapuo na World Bank zinataka
mtu/kampuni/kikundi kinachotaka kuanzisha benki ya biashara lazima kiwe
na mtaji wa bilioni 15 huku kiasi cha shilingi bilioni 2 zinahitajika
kuanzisha banki ya jumuiya. Hii sheria imechangia kushamili kwa mabenki
mpaka wataalam wakatahadharisha hekima na busara iliyotumika kuchochea
mabenki mengi kiasi hiki kwenye nchi yenye uchumi mdogo na tegemezi.
Taarifa ‘’feki’’ za Benki ya Dunia (WB) inaonyesha kuwa pato la
Mtanzania(Per capita income) kwa sasa ni dola za Marekani 900 mpaka
1,000 na kwa maana hiyo uwepo wa benki nyingi nchini ni sustainable
katika ukuaji wa uchumi.
Eti hata huyu Mama na familia yake ambao wanaishi katika kijiji cha
Mulumba, Kata ya Bwina, wilaya ya Chato, Geita kwa mujibu wa World Bank
tunaambiwa wana pato la dola 900 kila mmoja! Gosh. Mungu saidia waja
wako!
Kumbukumbu zinaonyesha Tanzania ni nchi ya 149 kati ya 157 kwenye nchi
zilizofanyiwa uchunguzi kuhusu ranking of happiness by country 2015 huku
Burundi ikishika nafasi ya 157.
Ukweli ni kuwa tuna mabenki mengi ambayo hayatoi huduma kwa wananchi wa
kipato cha chini lakini pia yalishatahadharishwa mapema kuhusu athari za
uwezekano wa kuingia kwenye matatizo yanayotokana na kutoa mikopo
ambayo uwezekano wake wa kutolipwa ni mkubwa.
Kwa kutumia msingi wa Non-perfomance Loans(NPLs), wataalam walikokotoa
asset quality based on the gross NPLs ratio na kugundua hatari iliyopo
mbele ya mabenki kwenye mikopo.
Tuna mabenki ambayo wataalam wa demand-pull wanaweza kusema,too much
money chasing too few customers na matokeo yake yanatoa mikopo kwa watu
ambao wahakidhi vigezo vya kibenki kupewa mikopo.
As a nation, We are sitting on volcano economy waiting to erupt!
Hili bomu kwa sasa limeanza kulipuka pole pole baada ya tabia za
kiuchumi zilizozoeleka kubadilishwa na utawala wa awamu ya tano.
Ni gharama kiasi gani zitaligharimu taifa kabla ya kuzaliwa njia imara
ya kiuchumi inayopaliliwa kwa sasa na serikali ya awamu ya tano?
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA