
Tarehe 23 ya mwezi wa tisa, Zari alifikisha umri wa miaka 36, na sherehe kubwa ilifanyika Zanzibar na Diamond kuoneka kufanya kufuru ya kumpa zawadi ya nyumba yenye thamani ya shilingi milion 18 za Kenya mlimbwende wake. Kilichokuja kushangaza, mama yake Diamond, Bi. Sandra Kassim hakumpa zawadi yoyote, wala hakumtumia ujumbe wowote wa kumtakia siku njema ya kuzaliwa. MAHENGA BLOG ikashtushwa na kuamua kufuatilia...
Siku tano baadaye, @kendrah-michaels (Sandrah Kassim) kama anavyofahamika kwenye mtandao wa Instagram alinukuliwa na blog yetu akimtakia siku njema ya kuzaliwa mlimbwende Wema Sepetu, mpenzi wa Diamond wa zamani, kitendo ambacho kimeonekana kumuumiza kwa THE LADY BOSS. Hawa ndiyo mastaa wetu wa nyumbani.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA