WACHEZAJI WA SIMBA WATOROKA HOTELINI MBEYA

Baada ya mechi iliyo shuhudia timu ya Simba ikipoteza alama 3 Muhimu dhidi ya Prisons FC ya jijini Mbeya, mtafaruku mkubwa ukatokea kwenye vyumba vya kubadirishia nguo uwanja hapo.


Inasemekana kuwa Viongozi wa ngazi za juu kabisa wa Klabu hiyo yenye makazi yake Jijini Dar mtaa wa Msimbazi wali waahidi wachezaji hao kuwa wangepewa Mishahara yao Kabla hawajaingia kwenye mechi yao dhidi ya Prisons FC, cha kushangaza kuwa kuna tetesi ambazo zilizopo chini kwa chini zinasema kuwa Baadhi ya viongozi hawa tayari kuwalipa mishahara baadhi ya wachezaji tu, na wala sio wote.

Baadhi ya wachezaji ambao inasemekana waliambiwa kuwa hawatopata mishahara yao kutokana na kuonyesha kiwango kibovu kwenye mechi dhidi ya African Lyon & Prisons FC ni Laudit Mavugo, Vicent Agban, Lufunga na Mohamed 'MO' Ibrahim.

Majira ya nyakati za Jioni kabisa baada ya mkanganyiko huu kutokea, baadhi ya wachezaji hao wameamua kuachana na kuondoka hotelini na kukodi usafiri binafsi kurudi Dar es Salaam kutokana na kile wanacho dai kufanyiwa ndivyo sivyo na viongozi wakuu wa Klabu hiyo. Mmoja wa wachezaji hao akiongea na mwandishi wetu aliyeko mbeya Lawrence Mwakipesile amesema ni bora warudi Dar ili wakae wajadili wafanye nini kuhusiana na suala hilo.

Tulipojaribu kuzungumza na Meneja wa kikosi hiko akasema 'Yeye hana mamlaka ya kuzungumzia suala lolote na waandishi wa habari hivyo tumfuate mhusika mwenye mamlaka ya kuzungumzia masuala ya klabu.

Mpaka tunaondoka jioni hii. Kambi ya Simba ilikuwa pungufu ya wachezaji 4, na waliobaki wengi walionekana kutokuwa na furaha na kile kinachoendelea kuhusu stahiki za wachezaji wenzao.

Chapisha Maoni

0 Maoni