DC BABATI: Ili kukuza uchumi wa nchi hii, watumieni wataalamu waliopo.

Mkuu wa Wilaya ya Babati Raymond Mushi.



Nchi kama Tanzania itaendelea kubaki nyuma katika uwekezaji kama haitowatumia wataalamu wenye fani katika uzalishaji ,hivyo Vyuo vya ufundi nchini vimeshauriwa  kuboresha mitaala ya masomo yanayofundishwa  ili kuzalisha wataalamu watakaoweza kuzalisha bidhaa bora  nchini zitakazoingia katika Soko la ushindani na kuifanya Tanzania kujivunia.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Babati  Bw. Raymond Mushi   juzi alipokuwa akimwakilisha  Mkuu wa mkoa huo Dokta Joel Bendera  katika mahafali ya tatu ya chuo cha ufundi VETA yaliyofanyika wilayani humo ambapo alisema kuwa  Mitaala hiyo ikilenga kutoa nafasi ya kujiajiri na kuajiri wengine maendeleo ya kweli yatafikiwa.

Alisema  maendeleo ni mjumuisho wa vitu vingi mbalimbali wakiwemo watu na stadi zao ambapo unapompa mtu stadi za kazi kama vinavyofanya vyuo mbalimbali  vya ufundi ambapo hutoa mafunzo  kwa wanafunzi wao ambao tayari inakuwa wamepata maendeleo ya nchi yatakayosaidia kukuza uchumi wa  viwanda katika nchi husika. 

Mushi  aliongeza kusema kuwa  ili kufikia  azma ya  uchumi wa viwanda kwa mwaka 2015 watanzania wanatakiwa wawe na uchumi wenye ushindani na kuwa na watu wenye ujuzi wa kutosha kwani raslimali kubwa kuliko zote katika uzalishaji  ni kuwa na watu wenye ujuzi. 

“Lazima vijana wajitambue na kujitathimini lengo la wao kuwepo katika dunia hii, itawasaidia kujua kipi cha kufanya na kipi kisichofaa kufanywa na hatimaye kuwa na ndoto za maisha wayatakayo kuishi, kwakuwa elimu inasaidia kujenga misingi bora ya maisha.” alisema Mushi. 



Mkuu wa Wilaya ya Babati Raymond Mushi akizungumza jambo katika Mahafali hayo.
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Manyara Bw, Felix Ole Ndukai akizungumza katika Mahafali hayo.


Mkuu wa chuo hicho Felix Ole Ndukai alisema kuwa chuo hicho kimekuwa kikiendesha mafunzo ya muda mfupi mafunzo ambayo yameisaidia jamii ya wana Manyara  kupata elimu na stadi za kazi  wengine wakiwa watumishi wa serikali na binafsi ambapo zaidi  ya wanafunzi2,400 wamepata mafunzo mbalimbali  kati ya hao 1,850 walipata mafunzo ya udereva pekee.

Mkuu huyo wa chuo aliyataja  baadhi ya mafunzo ya muda mrefu kuwa ni Uhazili,uungaji vyuma, useremala,uashi, umeme, maabara, ufundi magari na mafunzo ya muda mfupi ni  udereva wa magari na pikipiki, udereva wa gari za abiria,ushonaji,ufundi wa kitarakimishi(Computer maintenance). 

Alisema chuo hicho pia kimeimarisha mahusiano mazuri na taasisi zilizoko mkoani humo na kuweza kutengeneza madawati 1,153 ya shule za msingi kwa ushirikiana na jeshi la Magereza mkoa, utengenezaji wa viti na meza jozi (seti)300 kwa shule za sekondari kwa kushirikiana na ofisi ya RAS mkoa wa Manyara jambo ambalo anajivunia. 

Alifafanua kuwa katika mahafani hayo ya tatu jumla ya wanafunzi 80 wakiwemo wanawake  23 na wanaume 57 walihitimu mafunzo hayo kutoka katika fani za umeme(15),useremala(13),maabara(21) na ufundi magari (31). 

Alitaja baadhi ya changamoto  zinayokikabili chuo hicho kuwa ni upungufu wa mabweni,karakana na madarasa, uhaba wa nafasi ya mafunzo kwa vitendo viwandani,upungufu wa magari ya kufundishia udereva na upungufu wa walimu.
Wahitimu wakiimba Wimbo wa Pamoja wa kuaga.
Mkuu wa Wilaya Raymond Mushi akimkabidhi Cheti mmoja ya wahitimu

Chapisha Maoni

0 Maoni