"Hii ni shida yetu watanzania wote, wataalamu, viongozi wa serikali na pia wanasiasa. Kwanza tuko SLOW, sijui tunaogopa kutoa maamuzi? Sijui ni taaluma duni? Sijui ni nini? Mwekezaji DANGOTE, tuliahidi kumpa malighafi ya LIMESTONE kwa ajili ya kuzalisha SARUJI kwa unafuu mkubwa; tuliahidi kumpa ardhi kwa bei nafuu au bure;
tuliahidi kumpa gesi nyingi tena kwa bei nafuu; tuliahidi kumpa makaa ya mawe kwa wingi tena kwa bei nafuu; tuliahidi kumpa nafuu ya kodi na mengine mengi; mazingira yaliwavutia (Dangote na wenzake) sana.
Dangote wakavutika wakaja. Mimi (Dk. Kafumu) nikiwa Kamishna wa Madini wakati huo nilitimiza wajibu wangu wa kuwapa leseni ya utafutaji na uchimbaji wa LIMESTONE kadri ilivyohitajika. Nawashukuru sana STAMICO walinisikiliza na kiwanda kijajengwa. Awamu ya tano (ya JPM) imekuja na mambo mapya, ahadi zingine (kwa wawekezaji) zinasuasua, sijui ni nini!
Prof Mjebda (anamtaja Prof. mwingine kwenye Whatsup Group) anaweza kutuelimisha hapa. Kiwanda hiki kikubwa kikiimarika; manufaa ni makubwa ikiwa ni pamoja na nchi kupata kodi za kutosha; ajira zitapatikana; sekta ya majenzi (ujenzi) itaimarika; uchumi utaimarika.
Ni muhimu tuwahamasishe (wawekezaji) tuangalie matokeo ya muda mrefu na siyo haya ya haraka. Kiwanda kikifungwa shida ni yetu, hebu tuwe na mioyo ya kibiashara siyo siasa za uzalendo uchwara. Samahani sana "
Dkt. Dalali Kafumu,
Kamishna Mstaafu wa Madini (Tanzania),
Mbunge wa Igunga (wa sasa),
Kada wa CCM.
#Note; Nimehariri lugha kwenye maoni hayo ya kitaalamu ya Dk. Kafumu. Tujadili seriously.
JSM.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA