Na Mahenga Blog
FAMILIA ya mfanyabiashara Geofrey Mungai imetoa msaaada kwa watoto yatima zaidi ya 200 kutoka kituo cha Daily Bread Life Ministres cha Mkimbizi katika Manispa ya Iringa na wale wa kituo cha Tosamaganga katika wilaya ya Iringa Iringa wapewa msaada wenye nguo na chakula msaada wenye tmamani ya Tsh milioni 3 kwa ajili ya sikukuu ya Chrismas na mwaka mpya .
Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo Mungai leo
alisema imekuwa ni kawaida ya familia yake kila mwaka kusherekea sikukuu mbali mbali pamoja na watoto yatima kama sehemu ya kuikumbusha jamii kuwa na utamaduni wa kuwatazama yatima hao ambao tegemeo lao kubwa ni jamii inayowazunguka.
Mungai alisema kuwa suala la kulea yatima linapaswa kuwa ni jukumu la watanzania wote na kuwa ili kuwawezesha watoto hao kujisikia ni sehemu ya familia zenye wazazi ni vema jitihada za vituo vya yatima hapa nchini kuendelea kuheshimika zaidi.
Hata hivyo Bw.Mungai alisifu kazi nzuri inayofanywa na kituo hicho cha DBL katika kuendelea kuwalea watoto ha kimwili na kiroho na kuendelea kuwa miongoni mwa vituo bora vya kulea yatima katika mkoa wa Iringa.
Aidha aliwataka wananchi wengine kuendelea kufika katika kituo hicho na kusaidia kulea watoto hao kwa kutoa misaada mbali mbali kama njia ya kuwafariji na kuwalea watoto hao kuliko kuwaachia walezi wao pekee.
Hivyo alisema kwa mwaka huu amelazimika kutoa msaada wa nguo na chakula kwa kila kituo msaada wenye thamani ya Tsh milioni 1.5 na kuwa ataendelea kufanya hivyo kwa ajili ya watoto hao ili siku ya sikukuu nao waweze kufafana na watoto wengine ambao wanawazazi wao wote wawili .
Mkurugenzi mkuu wa kituo hicho mchungaji Mpeli Mwaisumbe Bw. Tukuswiga Mwaisumbe alisema kuwa kituo chake cha DBL kilichopo chini ya usimamizi wa mchungaji Neema Mwaisumbe kina watoto yatima 43 na kuwa maendeleo ya kituo hicho yametokana na jitihada za wadau mbali mbali ambao wameendelea kujitolea kusaidia kituo hicho.
Alisema kuwa mbali ya familia hiyo ya Mungai kuendelea kutoa msaada wakati wa sikukuu mbali mbali kwa watoto hao bado michango yake imeendelea kuwa chachu kwa wadau wengine kujitokeza kusaidia watoto hao kwa misaada mbali mbali .
Hata hivyo alisema kuwa wadau wanaoendelea kusaidia kituo hicho ni wengi zaidi na kuwa kwa umoja wao kituo hicho kinaendelea kuthamini michango yao na kuomba kuzidi kujitolea zaidi kwa ajili ya watoto hao kwa ajili ya kuona watoto hao wanapata elimu Kituo hicho ambacho kina zaidi ya miaka 15 15 toka kuanzishwa kwake kimefanikiwa kuanzisha shule yake ya Sekondari iliyopo kijiji cha Mgera ambayo inapokea na watoto wengine kwa kuchangia ada ndogo zaidi kuzindua shule ya sekondari .
kama umeguswa na jitihada za wale wote wanaojitolea kusaidia yatima wa kituo hiki cha DBL mkimbizi Iringa unaombwa kuchangia mchango wako wowote kupitia namba hii ya mkurugenzi mtendaji wa kituo hiki mchungaji Mpeli kupitia huduma ya TIGO PESA 0719239936 na M-PESA ni 0754362536 na Mungu atakubariki na kukuongezea pale ulipopunguza.
Aidha alishukuru ushirikiano kubwa ambao umekuwa ukionyeshwa na wadau mbali mbali kama mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na wadau wengine mbali mbali .
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA