Majasusi wa Marekani wauawa China


Gazeti la New York Times limeripoti kuwa China, imewauwa au kuwafunga jela majasusi kati ya 18 au 20 hivi wa CIA, katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na kulemaza kabisa shughuli za Marekani za kuichunguza China.


Afisa mmoja mkuu wa Marekani ameliambia gazeti hilo kuwa, hiyo ni mojawepo ya ukiukaji mkubwa wa usalama, kwa miongo kadhaa na kufananishwa na usaliti wa kutoa siri kwa Urusi na Aldrich Ames (wa CIA) na Robert Hanssen (wa FBI).

Baadhi ya watu sasa wanadhani kuwa China, ilidukua mfumo wa mawasiliano wa CIA, ambayo hutumiwa katika mazungumzo ya kisiri.

Lakini kunao wengine wanaoamini kuwa, mdukuzi alisambaratisha kizuizi cha siri cha wapelelezi wa Marekani, mnamo mwaka 2010.

Majasusi hao walianza kutoweka mmoja baada ya mwingine, kuanzia mwanzo wa 2011 (huku mmoja wao akipigwa risasi mbele ya wenzake katika eneo la kubarizi, kwenye jumba la serikali).
Idara ya ujasusi CIA, imekataa kuzungumzia swala hilo

Chapisha Maoni

0 Maoni