Hiki ndicho kilichompeleka Belle Tisa South Africa.

Meneja wa Belle 9 anayefahamika kwa jina la Jazz amefunguka mbele ya kamera ya eNewz sababu ya kufanya video ya Belle 9 nchini Afrika ya Kusini badala ya Tanzania kuwa ni kukosekana kwa "models" na waliopo wamekuwa wakitaka kiwango kikibwa cha pesa.

“Tumeamua kuifanyia video hiyo Afrika ya Kusini si kwamba maeneo ya nyumbani ni mabaya hapana bali mamodel wa hapa nyumbani wamekuwa na bei kubwa sana kuna wasichana wawili tuliwaambia wakasema bei zao ni milioni 2 tukashindwana nao tukaona tukafanye kazi na wale kule ambao unawalipa dola 100 tu kwa video moja”
Belle 9 ni kati ya wasanii ambao wameweza kukaa kwenye muziki kwa muda mrefu na bado anaendelea kufanya vizuri sana katika muziki wake na kwa sasa katika wimbo wake wa Give it to me ameamua kutumia vionjo kutoka katika wimbo wa Saida Karoli ili kunogesha zaidi muziki wake 

Chapisha Maoni

0 Maoni