"Wapiga dili" ni neno la Kiswahili kisicho rasmi linalomaanisha aina fulani ya watu waovu wanaotumia njia za kidanganyifu za kisomi au "kiujanja ujanja"kupitia nafasi zao za kazi kujipatia maslai binafsi fulani hasa ya kifedha kinyume na miongozo ya utumishi wao.
Fixed deposit account ni Akaunti maalum ya Benki inayotoa riba maalum mara nyingi kuanzia asilimia nne(4) mpaka kikomo cha chini cha riba kwa mwaka kwa mujibu wa Benki kuu kwa mtunzaji kama ataifadhi fedha hizo mpaka mwisho wa muda uliokubalika,
inatumika kuhifadhia fedha hasa zile ambazo haziitajiki kwa "immediate use" kwa kipindi cha miezi mitatu au zaidi.Mtunzaji fedha hupewa riba pale tu anapokidhi masharti ya akaunti hii hasa kutotoa fedha kwenye akaunti hii mpaka mwisho muda wa mkataba na anaposhindwa kutekeleza masharti haya anaweza kupoteza riba yake hasa pale anapoamua kuchukua fedha zake kabla ya muda uliokubaliwa kufikia kikomo.
Akaunti hii hutumiwa sana hasa pale kunapokuwa na kiasi kikubwa cha fedha kwenye "entity" ambacho matumizi yake yamesogezwa mbele ila hayaepukiki na hakuna mpango wa kupadilisha matumizi husika na uamuzi wa kuziifadhi fedha kwenye "fixed deposit account" ulenga hasa kupambana na kushuka kwa thamani ya fedha kutokana na "time value of money"na kupata angalau faida kidogo ambayo ni ndogo ukiliganisha na faida ambayo ingeweza kupatikana kama maamuzi ya kuziweka fedha hizo kwenye "risky Investment " au matumizi mengine muhimu yangekumbatiwa .
Siku za hivi karibuni Mkuu wa nchi aliivunja Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tazania (TRA) kutokana na sababu mbalimbali iliyotajwa ikiwa ni kitendo cha TRA kuifadhi makusanyo ya mapato kwenye "Fixed deposit account" kinyume na malengo ya kuanzishwa kwake.Nanukuu malengo ya kuanzishwa kwa TRA : 'The Tanzania Revenue Authority (TRA) was established by Act of Parliament No. 11 of 1995, and started its operations on 1st July 1996. In carrying out its statutory functions, TRA is regulated by law, and is responsible for administering impartially various taxes of the Central Government" source: Tanzania Revenue Authority - About TRA
Ni kweli kabisa kwamba fedha zilizopo kwenye "fixed deposit account" siyo rahisi kuibiwa na kama zikiiibiwa basi itakuwa ni sehemu nyingine na siyo katika mikono ya Benki husika na hata kama zikiibiwa pia ni raisi kuwafahamu wahusika kutokana na uwazi wa miamala ya kibenki.
"Wapiga dili" katika sekta za Umma na sekta binafsi hasa "CEOs" na "MDs" na"Board members" wanaweza kuamuru kiasi fulani kikubwa cha fedha cha "entity" husika kiwekwe kwenye "fixed deposit account" kwa manufaa yao binafsi na si kwa "entity" husika na kujipatia fedha nyingi kiundanganyifu kwa mgongo wa kuzitunza fedha vizuri kwenye akaunti hii maalum .Zifuatazo ni baadhi ya njia za "kupiga dili" kupitia fedha iliyowekwa kwenye "fixed deposit account" zinazotumiwa na watajwa hapo juu ambazo sio rahisi kugundulika:
1.Kugawana fedha na Wakuu wa Benki husika iliyopatikana kupitia "Profit based bonus plan": Wakuu wa Benki nyingi huwa kwenye mikataba yao ya ajira kuna kipengele cha kupata "Bonus" hasa pale wanapokuwa wamefikia kiwango cha faida iliyopangwa kupatikana katika mwaka wa fedha husika . Mabenki hupata faida kubwa kutoka kwenye "fixed deposit account" hasa zenye fedha nyingi ,riba ya chini na zinazokaa kwenye akaunti kwa muda mrefu na kusaidia kufikia "profit target", Kwa mfano wapiga dili wanaweza kuweka fedha kwa muda mrefu na riba ya chini sana kwenye "fixed deposit account" ukilinganisha na riba kubwa ambayo benki ingeweza kutozwa kwa kukopa kiasi hicho hicho cha fedha kutoka benki kuu au benki nyingine za biashara hivyo kwa sababu hii wakuu mabenki uingia dili maalum na wenye fedha nyingi hasa idara za serikali ili waweke fedha zao ummo kwa riba ya chini ili Benki iweze kuzizungushia na kupata faida kubwa. Halafu wapiga dili mgao wao wanaupata baada ya wakuu benki hao kupata "Bonus" na siyo rahisi "kutrace" miamala hiyo ya kugawana "Bonus" ambayo mara nyingi hufanyika kiusiri sana kwenye mahotel na mabaa makubwa kimya kimya na kwa uangalifu wa juu sana.
2.Kupewa cha juu (Tip) maalum:Baada ya kufanikishwa kuweka kiasi kikubwa cha fedha kwenye fixed diposit wapiga dili hupewa "special tip" na uongozi wa benki husika ambayo huwa haionekani kwenye miamala ya benki kwa kuwa hufichwa kwenye matumizi mengine hasa kwenye "corporate social responsibility" ,matumizi mengine yanayofanywa ili kuisaidia jamii au Ada fulani inayoweza kujitokeza katika mchakato wa kufanikisha ufunguaji wa akaunti hii maalum.
3.Kugawana hisa kupitia "Employees Share option plan" (Esops):"Wapiga dili" wanaweza kupata hisa za bure kutoka kwenye mgao wa hisa pale viongozi wa benki wanapopewa hisa kutokana na Benki kufanya vizuri huku "performance" ikichangiwa kwa kiasi kikubwa na fedha zilizopo kwenye " fixed deposit acccount".siyo rahisi kugundua uovu wowote kwani wahusika ujifanya wameuziana hisa lakini kunakuwa hakuna "exchange of cash or cash equivalents" kiuhalisia.
4.Biashara zao kukopeshwa kirahisi kwa "terms" nzuri au kupewa Kazi na Benki :"Wapiga dili" baada ya kufanikisha kuweka kiasi kikubwa kwenye "fixed deposit account" wanakuwa tayari wametengeza mazingira mazuri ya kufanya biashara na Benki husika kupitia mikopo yenye gharama nafuu au wakati mwingine biashara zao kupewa nafasi kutoa huduma kwa Benki. Benki huitaji huduma kama vile ulinzi,usafi,chakula na "shelter", ushauri wa kodi,ukaguzi wa fedha n.k na baadhi ya huduma hizi hutolewa na "Wapiga dili" kupitia kampuni zao zilizosajiriwa kupitia majina ya watu wengine au majina yao lakini hii ni nadra sana kutoka na kuofia kugundulika.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA