Jeshi la Polisi Wilayani Biharamulo wanachunguza tukio la mwanaume mwenye miaka 60 kujiua kwa kujinyonga kwa kujitundika juu ya mti kwa kamba ya katani.
Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Augustine Ollomi amesema marehehmu jina la Marehemu ni William Bizilege, mkazi wa kijiji cha Bisibo wilayani Biharamulo.
Kamanda Ollomi amesema wiki mbili zilizopita marehemu Bizelege alimuua mkewe kisha alikimbilia mafichoni na Jeshi la Polisi lilikuwa likimsaka. Polisi imesema alimuua mkewe sababu ya wivu wa mapenzi.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA